WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA MWONGOZO WA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA USTAWI WA JAMII

Na WMJJWM, Dodoma Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amezitaka Wizara zinazohusika na utekelezaji wa Mwongozo wa Mpango Kabambe wa Afua za Ustawi wa Jamii kuhakikisha zinasimamia urasimishwaji na utekelezaji wa mwongozo huo katika jamii. Hayo yamebainika wakati wa uzinduzi wa Mwongozo huo uliofanyika Leo Septemba 23 2022 jijini Dodoma.